Ni aibu iliyoje! Licha ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, njemba
mmoja ambaye jina lake halikufahamika, mkazi wa Raskazoni jijini hapa
amepokea kichapo ‘hevi’ baada ya kumharibia swaumu mke wa mtu ndani ya
daladala, Amani lina kisa na mkasa.
Njemba huyo akipokea kichapo toka kwa abiria waliokuwemo kwenye daladala hiyo.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu na kuacha mshangao
mkubwa kwa abiria huku wengine wakimwachia laana ya mdomo njemba huyo,
lilijiri mapema wiki hii ndani ya dalalada inayofanya safari zake kati
ya Sahare na Raskazoni ambapo mwanamke huyo alikosa siti hivyo
akalazimika kusimama. Shuhuda huyo alisema kuwa, ndani ya daladala hiyo kulikuwa na mbanano wa abiria ambapo njemba huyo alitumia fursa hiyo kujiridhisha baada ya kupata mfadhaiko kisha kumchafua mwanamke huyo aliyedai kuharibiwa swaumu yake kwa kuwa alikuwa amefunga.
...Wakizidi kumuadabisha.
“Jamaa tulimchukulia kama abiria wengine na kwa kuwa daladala ilikuwa
imejaza sana, muda mwingi alionekana kumsogelea yule mke wa mtu na
hatukujua kama alikuwa akitaka kumfanyia mchezo mbaya,aibu kweli”
alisema shuhuda huyo. Alitiririka kwamba, baada ya mwendo mrefu kidogo, njemba huyo alianza taratibu kufunua baibui la yule mke wa mtu na kuanza kumfanyia kitendo kichafu.
Mwanamke aliyefanyiwa kitendo hicho cha aibu akilia.
“Yule mke wa mtu mwanzoni aliona kawaida kugusana na abiria kutokana
na gari kujaa lakini alikuja kushtuka kama anavuliwa nguo ndipo
alipogeuka nyuma na kumkuta jamaa akiwa ameshikwa na mfadhaiko huku
akiwa amemchafua nguo yake sehemu ya nyuma. “Mke wa mtu ikabidi apige kelele ya kuhitaji msaada ndipo daladala ikasimama kituo cha Mabanda ya Papa na abiria wote tukamshusha na kuanza kumtembezea kichapo ambapo na yule mama alishindwa kujizuia na kuharibu swaumu yake kwa kumpiga,” alisema.
Hata hivyo, baada ya njemba huyo kupewa kichapo cha nguvu na raia waliomzingira, alifanikiwa kuchoropoka na kukimbilia eneo la ukuta na kutokomea akimuacha yule mama akiendelea kulia na kusema swaumu yake imeharibika.

Note: Only a member of this blog may post a comment.