Ukitaka kujua kuna watu hawana kazi ya kufanya utaangalia tofauti ya
comment za kwenye post ya Davido kwenye instagram. Kawaida huwa anapata
comment 100 hadi 200. Lakini post hii ambayo aliyoweka picha ya bendera
ya Tanzania imepata zaidi ya comment 2600 ndani ya masaa 4.
Ukiangalia comment zimejaa za wa Tanzania waki-comment ujinga kumpa
support na wachache wakiongea vitu vya msingi. Hapa ni hivi, kuna kundi
la watu wanaongoza kampeni za kumpigia kura Davido kwenye vipengele vya
MTV Awards ambapo Davido yupo na Diamond...Kisa cha Watu kumpigia Kura
Davido Kinatokana na Ugomvi wa Diamond na Wema Sepetu Ambao walikuwa ni
Wapenzi zamani...Wema Sepetu na Team yake ndio vinara wa kuwashawishi
watu wampigie kura Davido Badala ya Diamond..
Sasa inavyoonekana Davido alipata hizo taarifa na kutumia advantage kwa
ku-post bendera ya Tanzania na kuweka alama ya love. Basi kawateka wote
wasio na kazi wanaanza kupoteza muda wao. Wengine wanasema Davido
ka-show love tu kwa Tanzania. Anaanzaje kutoa love bila sababu ya
msingi.

Ishu za kitaifa tuache team zisizokuwa na msingi na tutumie bundle zetu
vizuri kama sio kujifunza mambo ya msingi basi kuwa support ndugu zetu
wanaotuwakilisha sio strangers. Hizi ni baadhi ya comments na nyingine
ni nzuri ila nyingine utashangaa kama kweli hawa ni watanzania au
wahamiaji tu.






Note: Only a member of this blog may post a comment.