Wednesday, June 17, 2015

Anonymous

WAFAHAMU MASTAA WALIOFUNIKA NA KUHARIBU KIMAVAZI KATIKA KTMA 2014/15 !

Muigizaji Wema Sepetu.
TUZO za KTMA zilitolewa Jumamosi iliyopita Mlimani City na kushuhudia msanii Ali Kiba akiondoka na tuzo tano peke yake.Jumla ya tuzo 26 zilitolewa usiku huo. Ukiachana na hiyo lakini pia kikubwa kilichotizamwa na wadau wengi waliojitokeza ni ishu ya mavazi.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mwana FA.
Baadhi ya walioonekana kuvutia wadau wengi waliokuwemo ukumbini hapo na hata wale waliokuwa wakitazama kupitia runinga.Muigizaji Wema Sepetu aliyekuwa na meneja wake, Martin Kadinda, walivutia wadau kwa kiasi kikubwa kwa namna walivyo vaa halikadhalika na Jokate Mwegelo.
Profesa Jay akiwa na mke wake.
Licha ya kutozoeleka kuonekana akiwa katinga gauni, kwa mara ya kwanza kwenye tuzo za KTMA 2014/15, Fetty  ambaye ni mtangazaji wa  Clouds Radio alitupia gauni la bluu bahari wakati akiongoza shoo ‘host’ sambamba na Zembwela aliyekuwa ndani ya suti, mwingine ni mtanashati Perfect Crispin wa Clouds FM.
Wengine walioonekana kutokelezea ni Mwana FA, Prof Jay na Kundi la Weusi hao wote walikuwa ndani ya suti za mikono mirefu. Wapenzi wa muda mrefu prodyuza, Nahreel na Aika nao walikuwa na mavazi yao yaliyowatoa ‘mwake’.
Martin Kadinda.
Aliojaribu kuvaa kama wasanii wa mamtoni na kuondoa utamaduni wa Kiafrika ni;  Msanii Bora wa Kike, Vanessa Mdee ambaye anafanya vizuri kimataifa kwa sasa kwa upande wa wadada alivaa nguo ambazo ziliacha kifua chake wazi sehemu kubwa.
Faiza Ally.
Faiza Ally alitoa mpya baada ya kushona nguo ya kitenge vipandevipande na kusababisha kuacha wazi eneo kubwa la mwili wake sambamba na ‘makalio’ kuonekana wazi licha ya kutinga na chupi ya kitenge. Wengine ni Queen Darleen na Linah Sanga nao walitupia nusunusu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.