NEW YORK, Marekani STAA wa
muziki wa Pop, Taylor Alison Swift amejivunia kumshauri staa mwenzake wa
muziki huo, Selena Gomez kujiweka mbali na Justin Bieber.
Taylor alikuwa rafiki wa karibu na Selena na ugomvi wao ulianza Mei
mwaka huu baada ya Bieber kumrudia Selena kabla hawajamwagana tena kwa
mara nyingine.
“Selena na Taylor kwa sasa ni marafiki wa nguvu. Anajivunia kumshauri
Selena na kufuata yale aliyokuwa akimsihi ya kujikita zaidi kwenye
muziki ambapo kwa sasa yupo katika mipango ya kutoka na albamu yake
inayoelezea mpasuko wa kimapenzi,” kilisema chanzo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.