Gari lililoporwa likiwa na matundu ya risasi.
MAJAMBAZI wanaokadiriwa kuwa watatu leo mchana wamefanya uporaji
kwenye maduka matatu ya kutoa na kuweka fedha kwa njia ya simu maeneo ya
Mikocheni Kwa-Mwalimu Nyerere jijini Dar ambapo baadaye walitoroka na
wawili kati yao kukamatwa.
Mashahidi waliokuwepo aneo husika walisema baada ya uporaji huo,
majambazi hao walipora gari aina ya Suzuki-Vitara na kuondoka nalo
lakini walipofika mita chache karibu na baa maarufu ya Rose Garden, gari
hilo liliwagomea kwenda na kuanza kupiga king’ora cha hatari (alarm)
kitendo kilichowafanya washuke na kuanza kutafuta njia nyingine ya
kujiokoa ambapo aliyeshika ‘fuba’ la fedha alifanikiwa kupora pikipiki
aina ya Boxer na kutokomea na wawili waliokuwa wakitafuta njia ya
kujinasua walitiwa mbaroni na askari polisi waliokuwa wakiwafukuza.
PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

Note: Only a member of this blog may post a comment.