Saturday, June 27, 2015

Anonymous

PICHAZ: DONALD NGOMA, MGHANA RASMI NDANI YA YANGA SC, WATUA BONGO LEO

Wachezaji wapya wa Yanga, Donald Ngoma (kushoto) kutoka Klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe na James Zutah kutoka Medeama ya nchini kwao Ghana , anayecheza nafasi ya beki ya kulia na kiungo, punde bada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo saa 3:30 asubuhi.
 
Zutah akihojiwa na mwandishi wa habari kabla ya kupanda gari kwenda kupumzika katika moja ya hoteli za kifahari katikati ya jiji walikoandaliwa na uongozi wa Yanga.
Mjumbe wa kamati ya Utendaji Yanga, Mussa Katabaro (kushoto mwenye kaptula), akiongoza msafara uliowapokea wachezaji wapya wa klabu hiyo, Donald Ngoma na James Zutah kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo
 
Ngoma na Zutah wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Yanga waliowapokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyerere leo asubuhi. Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha (wa pili kulia), Katabaro na Mjumbe wa Kamati ya mashindano, Ndama (wa pili kushoto)
 
Gari lililowachukua Ngoma na Zutah lililokuwa likiendeshwa na mjumbe wa kamati ya Utendaji, Katabaro kwenda kupumzika kabla ya taratibu za kuwasainisha kufuatia.
(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)A

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.