MUNGU
wangu! Mwanaume mmoja mkazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam
aliyefahamika kwa jina moja la Salum, anasakwa na polisi kwa tuhuma za
kumbaka na kumpa ujauzito bintiye wa kambo (jina limehifadhiwa).
Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti hili kuwa mwanaume huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaye kwa muda mrefu, lakini iligundulika hivi karibuni baada ya wawili hao kufanya jaribio la kutoa mimba hiyo ili msichana huyo aendelee na masomo katika shule moja ya sekondari iliyopo mkoani Iringa.
Mama wa binti huyo, Prisca Steven (32) alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema licha ya kupata aibu kubwa, lakini pia mwanaume huyo ameharibu maisha ya mtoto wake kwa kumkatisha masomo. Alisema kwa sasa mumewe huyo amekimbia nyumbani na amekuwa akimtumia sms za vitisho au kuomba afute kesi hiyo ili kuepuka kifungo cha miaka 30 jela endapo atakutwa na hatia.
Gazeti hili lilifanikiwa kumpata binti huyo kwa njia ya simu ambaye alikiri kupewa ujauzito na baba yake wa kambo, lakini akisema mwanaume huyo alimlazimisha na kumwingilia kwa nguvu wakati mama yake akiwa hayupo nyumbani.
Kwa upande wake, mwanaume huyo alipoulizwa kwa njia ya simu, alikana kuhusika na tukio hilo akisema hausiki na kwamba hajakimbia nyumbani kwake isipokuwa alipata safari ya kikazi huko Zanzibar. Jalada la shauri hilo limefunguliwa katika Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa nambari KJN/RB/6485/15 KUBAKA.

Note: Only a member of this blog may post a comment.