Saturday, June 27, 2015

Anonymous

MBUYU TWITE: Hawa Madogo Hatari Sana!

Nassor Gallu, Dar es Salaam
BEKI kiraka wa Yanga, Mnyarwanda, Mbuyu Twite, amewaangalia wachezaji wapya wa kikosi hicho, kisha akasema: “Hawa madogo hatari sana jamani.”

Twite, raia wa Rwanda mwenye asili ya DR Congo, amesema hayo baada ya kufanya mazoezi na wachezaji wapya wa Yanga kwa siku chache tu na kukubali kwamba watakuwa wakali katika mechi zao.
Hapo alikuwa akiwazungumzia Malimi Busungu, Deus Kaseke, Geofery Mwashiuya na Mwinyi Haji ambao wamesajiliwa na Yanga kutoka timu za Ligi Kuu Bara na Zanzibar. 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Twite anayemudu kucheza zaidi ya nafasi mbili uwanjani, alisema kwa siku chache alizocheza mazoezi na wachezaji hao anaamini watakuwa msaada kwao katika kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.