


Hali ya taharuki imejitokeza katika ofisi kuu za CCM mkoa wa Ruvuma wakati wa kusubiri ujio wa mbunge wa Monduli na mtia nia ya urais mh.Edward Lowassa, kundi la madereva bodaboda lilijikusanya na kuvamia katika ofisi hizo na kudai pesa hali iliyosababisha sintofahamu miongoni mwa watu waliohudhulia. Awali kiongozi wa itifaki katika ujio huo alitangaza kuwa hakutakuwa na pesa zozote za Lowassa na hivyo kuwataka wenye mapenzi ya dhati kumuunga mkono!

Note: Only a member of this blog may post a comment.