Tuesday, June 16, 2015

Anonymous

Aunt Ezekiel Kuja na Hii Baada ya Kujifungua!

Baada ya hivi karibuni kupata jina jipya la mama cookie, staa wa bongo movies, Aunt Ezekiel amesema amejipanga kurudi kwa kishindo kwenye bongo movies baada ya lengo lake hilo kutimia.

Akizungumza na gazeti la Nipashe Aunt amabaye amejifungua mwezi uluopita alisema amejipanga kutoa filamu amabayo itahusu maswala ya wazazi ili kueleimisha wanawake wenye tabia ya kutupu watoto wachanga mara baada ya kujifungua.

Aidha amesema huchukia wanaume wenye kuwapa mimba wanawake kisha kukataa kuhusika katika malezi ya mtoto aliyezaliwa.

Hivyo, alisema anajipanga kutoa elimu kuwa uzazi ni wakuheshimiwa na hususan kwa wanaume.
Aunt yupo katika maandalizi ya filamu hiyo ambayo atawashirikisha wasanii wakubwa na chipukizi alisema.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.