Sunday, May 17, 2015

Anonymous

VIDEO: Mashambulizi kwa wageni Afrika Kusini bado ni ishu kubwa, hii ni ripoti nyingine kutoka huko!

Xenophobia-In-South-Africa-Nigerians-Victims-650x398
Stori ya ishu ya ubaguzi Afrika ikarudishwa kwenye headlines na matukio ya South Africa.. Xenophobia ikachukua nafasi ripoti nyingi za habari kubwa Afrika kwa zaidi ya mwezi mmoja, kwa sasa hivi ni kama hali imetulia japo sio kwa asilimia 100 !! 

Wenyeji wanahofu kuendelea kuwepo Afrika Kusini, hii imeripotiwa na kituo cha TV  cha SABC Afrika Kusini, wageni wengine 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliamua kuanza safari ya kurudi kwao ikiwemo Wamalawi. 

Watu zaidi ya 100 walilazimika kurudi kwenye nchi zao kutokana na kuanza kwa vurugu za mashambulizi ya wenyeji wa South Africa waliokuwa wakiwafukuza wageni.. wengine waliuawa na wapo waliojeruhiwa na kupoteza mali zao pia kutokana na mashambulizi hayo. 

Nataka nirudi nyumbani kwa sababu huku hali sio nzuri.. wanatupiga, wanataka kutuua nimeona nirudi tu nyumbani“– Hassan Shalifa, mmoja ya raia wa kigeni waliokuwa wakijiandaa kuondoka South Africa.
Tazama video hiyo kwa kubonyeza play au download hapo chini....

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.