Na Valence Robert, Geita.
Kikao cha kamati ya halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM), wilaya ya Geita kimemtimua katibu msaidizi wa wilaya hiyo Patrick Kusaga kwa kile kinachodaiwa kutafuna fedha za mapango ya nyumba ya chama hicho zaidi ya sh. Milioni 6.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mkutano wa chama hicho katibu mwenezi wa wilaya Jonathan Masele, alisema wamefikia maamuzi hayo ya kumuondoa na kufunga ofisi yake kwa ubadhilifu mkubwa wa fedha na dharau kwa viongozi wenzake.
Masele alisema kamati ya siasa ya wilaya imekuwa ikimwita mara kwa mara ili kuzungumzia tuhuma zake lakini amekuwa akiwatolea majibu ya kejeli, jambo ambalo limepelekea kumuondoa.
“Tumefikia maamuzi haya kutokana na Katibu huyu msaidizi kujiona yeye ni zaidi ya wenzake na kujipa madaraka makubwa na amehusika na upotevu wa sh. Milioni 6 za kodi kutokana na hayo, kamati ya siasa ya wilaya imemwita mara kadhaa lakini ameshindwa kutii wito na amekuwa akitutolea lugha za kejeli kuwa sisi hatuwezi kumfanya chochote kwa kuwa anawakubwa ambao wanamlinda”.
“Kamati ya siasa ya wilaya hatumtaki labda Mkoa au makao makuu wampeleke wanakojua wao lakini hapa hatumhitaji, anasababisha chama kiyumbe na anaweza kusababisha chama tulikose hili jimbo la Geita, tumeamua kufunga na ofisi yake hapa tunasubiri kuletewa mtu mwingine huyu hafai kabisa kuwa hata balozi kwa ufisadi wake.. kadi za ccm tunaziuza sh. 300 lakini yeye anaziuza sh 540 kinyume na utaratibu,.”alisema Masele.
Waandishi wa habari walilazimika kumtafuta Patrick Kusaga ili kujua tuhuma hizi zinazomkabiri ni za kweli ama la, alisema yeye hajui lolote juu ya hilo na alikuwa Butiama kwenye msiba wa mtoto wa Mwl. Nyerere.
“Hizo tuhuma mimi sizijui na sijaitwa na tunapoongea nipo Mwanza natoka Butiama kwenye msiba wa mtoto wa mwl. Nyerere’’alisema Kusaga.
Hata hivyo mara baada ya waandishi wa habari kumaliza kuongea na Kusaga, Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Geita Joseph Msukuma alipiga simu kwa mmoja wa waandishi akimtaka asiandike chochote juu ya habari hiyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.