Sunday, May 17, 2015

Anonymous

MLIPUKO WA BOMU WAUA WATATU HUKO KABUL -PICHAZ

Baadhi ya magari yaliyoteketea kutokana na shambulio hilo.
Mmoja wa majeruhi katika shambulio hilo akitolewa eneo la tukio.
Mama huyu akitolewa eneo la mlipuko na kupelekwa sehemu salama.
WATU watatu wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine takribani 20 wakijeruhiwa baada ya mlipuko kutokea kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Kabul nchini Afghanistan leo.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa mlipuaji wa bomu hilo la kujitolea muhanga alikuwa amelenga wanajeshi wa kimataifa nje ya lango kuu la uwanja huo wa ndege. 

Lango hilo hutumika na vikosi vya kijeshi vya kigeni. Kundi la Taliban limethibitisha kuhusika na shambulio hilo katika taarifa yake lililoituma kwa wanahabari.

Shambulizi hilo linafanyika ikiwa ni siku tatu baada ya mwanamgambo mmoja wa Taliban kuwaua watu 14 wakiwemo raia tisa wa kigeni katika hoteli moja mjini humo.
Chanzo: BBC

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.