Monday, May 18, 2015

Anonymous

MGUU WA JINI: LIONEL MESSI Aipa Ubingwa FC Barcelona Baada ya Kuwanyuka Mabingwa Watetezi Atletico Madrid! #LaLiga

Baada ya kukata tiketi ya kucheza fainali ya UEFA Champions League mapema wiki hii, leo hii klabu ya FC Barcelona imetawazwa rasmi kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Hispania.
Barcelona wametazwa rasmi kuwa Mabingwa wa La Liga baada ya kuwafunga waliokuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Atletico Madrid katika mchezo uliomalizika hivi punde.

Lionel Messi alifunga goli pekee lilowahakikishia Barca ubingwa huo katika dimba la Vicente Calderon.

Ubingwa huu unakuwa wa 23 katika historia ya klabu hiyo ya Catalunya.
Barca watakabidhiwa kombe lao watakapocheza mchezo wa mwisho wa ligi wiki ijayo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.