Wakati FC Barcelona wakitawazwa kuwa mabingwa wa mara ya 23 wa ligi kuu yaHispania, Real Madrid walikuwa ugenini huko mjini Barcelona kucheza dhidi ya Espanyol..
Cristiano Ronaldo alitengeneza na kuvunja rekodi nyingine usiku wa
leo, baada ya kuweka rekodi ya kufunga hat tricks nyingi zaidi katika
historia ya la Liga(26) baada ya leo kufunga magoli matatu kati ya manne
yaliyofungwa na Madrid vs Espanyol.
Hat trick ya leo pia ni ya saba kwa Ronaldo msimu huu wa Laliga – hakuna anayemfikia kwenye hilo.
Ronaldo pia leo ametimiza jumla ya magoli 57 katika mashindano yote
msimu huu – kati ya hayo 45 ni katika La Liga pekee na hivyo kumfanya
kuwa mfungaji bora mbele ya Messi mwenye 41.
Goli
lingine la Real Madrid kwenye mchezo huo lilifungwa na Marcelo baada ya
kupokea pasi nzuri kutoka kwa Cristiano Ronaldo – hii pia assist ya 22
kwa Mreno huyo msimu huu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.