Haruni Sanchawa
NI maajabu ya mwaka! Almas Hassan mkewe Joyce Ezekiel wanadaiwa kuwatelekeza watoto wao saba huko Kigogo Fresh, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugumu wa maisha, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.
Kwa mujibu wa chanzo, wanandoa hao wawili walikuwa wakiishi Kigoma pamoja na watoto wao nane, lakini miaka mitatu iliyopita mume aliondoka nyumbani na kumuaga mkewe kuwa anaenda kutafuta maisha jijini Dar, ambapo alifikia Kigogo Fresh.
“Alipofika hapa alisema yeye ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na alitafuta hifadhi na kupata kutoka kwa bwana mmoja ambaye alimpa nyumba yake ili pia aweze kumlindia. Hakuwahi kusema kama alikuwa na familia huko alikotoka na akawa anajishughulisha na useremala,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuishi kwa muda wa miaka mitatu bila mumewe, inadaiwa kuwa mke akiwa na watoto wake wote walifunga safari kwenda Dar ambako alidokezwa kuwa mumewe alikuwa akiishi huko Kigogo Fresh na alipofika, alipokelewa na mumewe huku majirani wakishangaa kufahamu kuwa ‘mgeni’ huyo alikuwa na familia kubwa kiasi hicho.
Inadaiwa kuwa Septemba mwaka jana, mama huyo aliondoka nyumbani hapo akimwambia mumewe kuwa hii ilikuwa ni zamu yake ya kulea watoto na kama utani, akatoweka nyumbani hapo bila kujulikana alipoelekea. Baada ya kuishi nao, Machi mwaka huu, Almasi aliwaaga watoto wake saba (mmoja mkubwa anadaiwa kutorokea Bagamoyo) kuwa anakwenda kumtafuta mama yao, lakini tangu siku hiyo hajaonekana tena, kitendo kilichosababisha familia hiyo kuishi kwa kuombaomba.
Inadaiwa familia hiyo iligeuka kuwa mzigo kwa majirani, hasa baada ya hivi karibuni mtoto wa mwisho mwenye umri wa miaka mitatu kupatwa na homa kali, ambapo baada ya kumfikisha hospitalini, alibainika kusumbuliwa na njaa baada ya kukaa siku tatu bila kula.
Gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto, Sophia Simba ambaye alipoulizwa suala la watoto hao alisema wazazi hao wanapaswa kutafutwa na kukamatwa kisha kushtakiwa kwa sababu kitendo walichokifanya ni kosa la jinai.
Watoto hao waliotelekezwa ni Fredrick Almas (18), Ezekiel Almas (16), Jenifar Almas (14), Eliza Almas (12), Frank Almas (10) Mariam Almas (6), na Hassan Almas mwenye umri wa miaka mitatu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.