CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo kimetoa taarifa yake
juu ya utaratibu utakaotumika katika uteuzi wa wagombea ndani ya chama
hicho kwa mwaka wa 2015.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa
Chadema Zanzibar, Salum Mwalim ametaja mchakato wa uteuzi kuwa
utahusisha hatua tatu katika ngazi ya kata na jimbo au wilaya na hatua
moja katika ngazi ya kitaifa.
Mwalimu alisema kuwa ngazi ya kwanza ni Mkutano Mkuu wa Jimbo ambao
utafanyika siku moja kwenye eneo moja au Makao Makuu ya Jimbo au eneo
ambalo litaamuliwa na vikao vya chama, wagombea kujipigia kura wenyewe
na kamati ya utendaji ya jimbo ambayo kazi yake itakuwa ni ya uteuzi wa
awali kwa mujibu wa katiba ya chama na kuwasilisha mapendekezo yake kwa
Kamati Kuu.
Aidha, aliongeza kuwa katika utaratibu huu wa mchakato wa kuwapata
wagombea, chama hakitaingilia mamlaka waliyojiwekea na Umoja wa Katiba
ya Wananchi (UKAWA) na kwa sasa tayari wale wote wanaohitaji kuchukua
fomu za kuwa wagombea, wanaweza kuchukua katika tarehe iliyopangwa
(ratiba ipo chini).
Aliongeza kuwa, fomu hizo zitaanza kuchukuliwa katika majimbo ambayo
hayana wawakilishi wao Bungeni ambapo majimbo yenye wawakilishi, fomu
zitaanza kutolewa hadi hapo Bunge litakapokuwa limevunjwa na mchakato
mzima wa utoaji fomu ukiwa tayari umehalalishwa.
Alitaja viwango vya fomu vitakavyotumika katika kugombea ngazi ya urais hadi udiwani kwa upande wa urais ni Sh.1,000,000, ubunge Sh.250,000 pamoja na viti maalum. Udiwani wa kata ni Sh. 50,000 pamoja na udiwani wa viti maalum.
Hivyo fomu hiyo itarejeshwa kwenye jimbo au kata ambayo mgombea
anagombea na ndipo atapaswa kulipia gharama za fomu husika baada ya
kuijaza na pia fomu zitapatikana katika ‘website’ ya chama ambayo ni www.chadema.or.tz
PICHA/STORI: DENIS MTIMA/GPL.
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDEKELEO
(CHADEMA)
RATIBA YA UCHUKUAJI FOMU, VIKAO VYA UCHUJAJI NA UTEUZI WA WAGOMBEA NDANI YA CHAMA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015.
18/05 – 25/06/2015
|
Kuchukua na kurejesha fomu za Udiwani Kata ambazo hatuna Madiwani.
|
Makatibu Kata/Jimbo na Wilaya
|
01/7 – 10/7/2015
|
Kuchukua na kurejesha fomu Kata ambazo tuna Madiwani.
|
Makatibu Kata/Jimbo na Wilaya.
|
15/7 – 20/7/2015
|
Uteuzi wa mwisho Wagombea Udiwani Kata pamoja na wale wa Viti maalum.
|
Kamati Tendaji za Majimbo.
|
18/5 – 25/6/2015
|
Kuchukua na kurejesha fomu za Ubunge Majimbo ambayo hatuna Wabunge kwa sasa, pamoja na Fomu za Ubunge wa Viti Maalum.
|
Makatibu wa Majimbo, Wilaya, Mikoa na Makao Makuu.
|
6/7 – 10/7/2015
|
Kuchukua na kurejesha fomu za Ubunge Majimbo ambayo tuna Wabunge kwa sasa.
|
Makatibu wa Majimbo na Wilaya.
|
20/7 – 25/7/2015
|
Uteuzi wa awali wagombea Ubunge.
|
Kamati Tendaji za Majimbo.
|
20/7 – 25/7/2015
|
Kuchukua na kurejesha Fomu za Mgombea Urais.
|
Makao Makuu
|
1/8 – 2/8/2015
|
Uteuzi wa mwisho wa Wagombea Ubunge kufanyika.
|
Kamati Kuu Taifa.
|
3/8/2015
|
Baraza Kuu Taifa
|
Kamati Kuu
|
4/8/2015
|
Mkutano Mkuu Taifa
|

Note: Only a member of this blog may post a comment.