Thursday, May 28, 2015

Anonymous

Hii leo inamhusu mlemavu kufanya utapeli wa pesa jijini Dar.. #Hekaheka (Audio)

OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Utapeli ni ishu ambayo iko sana mjini.. wakati mwingine unatapeliwa na mtu ambae hata hukutarajia, jamaa mmoja ambae anafanya biashara ya kuuza magari ametapeliwa na mtu ambae ni mlemavu Dar. 

Kukutana kwao ilitokana na dalali mmoja ambae aliwaunganisha ili wauziane gari, baadae wakaenda Benki Kariakoo ambako alidai kwamba alitumiwa pesa na wafadhili wake walioko nje ya nchi. 

Ikashindikana kutoa pesa kwa sababu alikuwa hana account ya dola, ikawa kunatakiwa pesa ili taratibu za kufungua account zikamilike.. huyo jamaa akatoa pesa hizo pamoja na pesa nyingine nyingi kumhudumia hoteli na vitu vingine wakati wanasubiri account hiyo ifunguliwe. Story ni ndefu, timu ya #LeoTena wamesema hii Hekaheka itaendelea kesho ili tusikie jinsi utapeli ulivyofanyika.. iliyosikika leo sehemu ya kwanza unaweza kuisikiliza hapa...

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.