Miaka karibu minne iliyopita Lowassa alijitahidi kujitetea kutokuhusika kwake na Richmond. Hoja za jana Jumatatu si mpya. Mwakyembe alijibu wakati ule; sijui kama leo atakuwa na majibu tofauti ya hoja za Lowassa.
Bonyeza Hapa Chini Umsikilize Mwakyembe... Wakati huo, mchambuzi wa siasa Julius S. Mtatiro anasema:
Ndugu zangu, Nilipofanya uchambuzi wa kina juu ya Edward Lowassa nilieleza Udhaifu wake katika maeneo mawili:
Kwanza nilieleza alivyo karibu na watu wenye majina na taswira zinazotia mashaka (tunawafahamu) na baadhi yao wamewahi kutuhumiwa kuhusika kwenye kashfa kubwa za ufisadi. Nikasisitiza kuwa kama hatatoa maelezo ya kuridhisha juu ya mgongano wa kimaslahi juu yake na wafanyabiashara hao wenye taswira hasi, atapata matatizo.
ALIPOONGEA NA WAANDISHI JANA KALIONGELEAJE HILI?
Pili, nilieleza kwamba hajawahi kuonekana akipambana na rushwa na wala rushwa, wala huwa hapendi kuongea mikakati ya kudhibiti rushwa n.k. Na nilisisitiza kuwa alipokuwa Waziri Mkuu hakuonekana mstari wa mbele kupambana na wala rushwa, nilionesha wasiwasi wangu juu ya uwezo wake wa kuondoa rushwa na wala rushwa wanaoitafuna nchi hii.

Tatu, nilitaja mambo matano yanayoweza kumwangusha kwenye mchakato wa uteuzi ndani ya CCM:
Moja, nilisisitiza juu ya makundi kama sababu ya kwanza ikitokea anaenguliwa.
Pili, nikazungumzia kashfa ya Richmond ambayo mara kadhaa amesikika akisema yeye hakuhusika lakini hakuwahi kuwataja waliohusika.
Tatu nilizungumzia historia ya CCM kutowahi kumpitisha kiongozi ambaye amewahi kutuhumiwa kimaadili.
Nne, nilizungumzia suala la afya yake.
Tano, nilizungumzia suala la yeye kujitolea sana kifedha kila anakoenda na kualikwa na nikaweka shaka juu ya fedha hizo kama zinatolewa ili kuwasaidia watanzania tu au ni moja ya njia ya kusaka ukuu.
Na mwisho, (Sita) niliongelea tetesi zilizopo kuwa yeye na bwana mkubwa hawana mahusiano mazuri hivi sasa.
JE ALIPOONGEA NA WAANDISHI JANA KAONGEA LOLOTE KATI YA HAYA?

Note: Only a member of this blog may post a comment.