Na Martha Mboma, Dar es Salaam
LICHA ya kuwa mkongwe, huenda neema bado inamfuata kipa Juma Kaseja aliyetemwa Yanga kutokana na Klabu ya Stand United kuweka nia ya kumsajili kwa dau la shilingi milioni 40.Stand United inataka kusajili kipa mkongwe na tayari jina la Kaseja ambaye kabla ya kutua Yanga aliichezea Simba kwa kipindi cha misimu 10, ndilo linaloonekana la kwanza kwao.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United, Muhibu Kanu, alisema wanaamini Kaseja atakuwa msaada kwao, hasa katika suala la kuongeza thamani ya timu yao.Kanu alisema kuwa, kwa sasa wamejipanga kuhakikisha wanamnasa kwa kiasi chochote kile cha fedha na kumpatia mshahara mnono ambao atauhitaji.
“Tulisema tangu kitambo kuwa tutafanya juhudi kuhakikisha tunainasa saini ya Kaseja, tumetenga kiasi cha shilingi milioni 40 na hata kama akisema tuongeze kidogo, inaweza kuwa zaidi ya hapo na sisi tutaweka rekodi.
“Tutamtimizia kile ambacho atahitaji, hususan kwenye mshahara, anaweza kupata zaidi ya ule wa Yanga na kwa sasa tunazungumza na meneja, tunaamini Kaseja ana uwezo mzuri na ataisaidia timu yetu msimu ujao, kutokana na msimu uliomalizika kipa na safu yote ya ulinzi kuruhusu mabao mengi sana, jambo ambalo lilituweka kwenye wakati mgumu,” alisema Kanu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.