Hatimaye ligi kuu ya England inaelekea kufikia tamati huku vita ya vilabu vya Man City, Arsenal na Man United ya kujihakikishia nafasi ya pili na ya tatu ikiwa nayo inaelekea mwishoni.
Mapema hivi leo City walijihakikishia kumaliza ndani ya top 3 baada
ya kuwafunga Swansea 4-2 na kuziacha United na Arsenal wakipambana
kuwania nafasi mojawapo kwenye top 3.
Vilabu hivyo muda mfupi uliopita vilikuwa vinatoana jasho katika
dimba la Old Trafford na matokeo ya mchezo yameipa Arsenal uhakika wa
kumaliza kwenye aidha nafasi ya pili au tatu kwenye Barclays Premier
League.
Mechi hiyo imemalizika kwa matokeo ya sare ya 1-1 kwa United na Arsenal.
Ander Hererra alifunga goli zuri katika kipindi cha kwanza cha mchezo
huo ambao kilikuwa kimetawaliwa na United kabla ya Arsenal kurudi
kipindi cha pili na kusawazisha goli hilo kupitia Tyler Blackett
aliyejifunga.
Kwa matokeo hayo Arsenal ambao wana mechi mbili mkononi wanaendekea kushika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 71 na United wana mchezo mmoja wakiwa na pointi 69.

Note: Only a member of this blog may post a comment.