Friday, April 24, 2015

Anonymous

Ugonjwa wa macho mekundu Dar, mapya uchaguzi mkuu TZ 2015 na biashara ya madini nchini …#PBCloudsFM


listen-now
Ijumaa ya April 24 nakukaribisha tena mtu wangu POWERBREAKFAST ya Clouds FM imefanya uchambuzi wa story zote kubwa kwenye kurasa za Magazeti TZ leo..
Ugonjwa wa macho mekundu umeibuka katika maeneo mbalimbali Dar, NEC imetangaza zabuni ya ununuzi wa vifaa vitakavyotuka kupigia kura, Polisi Bariadi wamesema kuwa kada wa CCM Ahmed Ismail ndio alirusha risasi ili kuwatawanya watu waliokuwa wameziba njia, Mbunge Augustino Mrema amesema ni ndoto kwa vyama vya upinzani kuishinda CCM, watuhumiwa 57 wanaodaiwa kodi ya majengo wamefikishwa kwenye baraza la ardhi na nyumba Wilaya ya Kinondoni na mgodi wa dhahabu Buzwagi kufungwa kutokana na uzalishaji kushuka. 

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ambae amezungumzia kuhusu wachimbaji wadogo wanaofanya kazi katika migodi na machimbo pamoja na soko la biashara ya madini nchini pia kulikuwa na mazungumzo na Mbunge Augustino Mrema ambae amezungumzia Afya yake pamoja na muenendo wa siasa katika jimbo lake. 
Bonyeza play hapa chini kusikiliza story zote…
-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.