Tuesday, April 21, 2015

Anonymous

SIMANZI: Mwanafunzi darasa la nne ajinyonga chumbani jijini Dar

Simanzi zimetawala katika familia ya mtoto Festo Filbert mwenye miaka 11 iliyopo Majohe kwa Ngosoma, Dar es salaam baada ya mtoto huyo kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali.
Tukio la kujinyonga kwa mtoto huyo aliyekuwa akisoma darasa la nne katika shule ya Msingi Pugu limeacha huzuni kwa majirani na ndugu zake ambao walikuwa karibu na mtoto huyo. 

Mtoto huyo alifikia maamuzi hayo juzi katika maeneo hayo ambapo alikutwa chumbani kwake akiwa amejinyonga na mwili wake ukiwa umeng’inia kwenye mkanda alioufunga shingoni.
Baadhi ya wananchi waliokuwa wakiishi karibu na mtoto huyo walisema wameshtushwa na kifo chake kwani  kabla ya kufikia uamuzi huo alionekana akicheza na wenzake. 

Walisema jumapili asubuhi alikwenda kanisani, na aliporudi alikuwa akichezana wenzake lakini walishangazwa na taarifa za kwamba amefariki baada ya kuamua kujinyonga. 
Hata hivyo haikuwa rahisi kufahamu sababu za kuamua kujinyonga na sasa maiti yake imehifadhiwa katika hospitali ya Amana huku upelelezi wa Polisi ukiendelea

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.