Thursday, April 23, 2015

Anonymous

MSIBA: MWANAMUZIKI MKONGWE TANZANIA AFARIKI DUNIA!

Marehemu Mutombo Lufungula Audax (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na Kasongo Mpinda.
MWANAMUZIKI na mtunzi mashuhuri wa Bendi ya Maquis Original, Mutombo Lufungula Audax, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, huko Kimara-Michungwani jijini Dar es Salaam.
Mwili wake umepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Audax alikuwa mmoja wa wanamuziki asili wa Kundi la Maquis Du Zaire. Kundi la Maquis lilianzia katika mji wa Kamina, Jimbo la Shaba, huko Kongo.
 Awali kundi hilo lilianza kwa kuitwa Super Teo, kisha kubadili jina na kuitwa Rocken Success na baadaye Super Gabby na mwisho wakati wakiingia Tanzania mwaka 1972 walikuwa wakiitwa Maquis Du Zaire.

Kundi hili la awali likuwa na wanamuziki tisa, na sasa baada ya kifo cha Audax, aliyebakia hai ni mmoja tu, Nguza Viking ambaye naye yuko kifungoni akitumikia adhabu ya kifungo cha maisha.
Mzee Audax alianza matatizo yake ya kiafya mwaka 2005 baada ya kupooza iliyomfanya apooze upande mmoja wa mwili. Amekuwa akilelewa na wanae kwa muda wote huo kutokana na kutoweza kuendelea na kazi.
Baadhi ya nyimbo alizotunga marehemu ni Kisebengo, Mpenzi Luta, Mimi na nyingi sana nyinginezo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.