Thursday, April 23, 2015

Anonymous

BABA 'AKE ZITTO KABWE Afunguka Mazito Kuhusu Mwanaye

Baba mzazi wa kiongozi wa ACT –wazalendo, Zuberi Kabwe, amesema pamoja na misukosuko ya kisiasa inayompata mtoto wake, Mungu ndiye anayemsimamia. 

Amesema kwamba kwa kuwa yeye ndiye mzazi wa mwanasiasa huyo amekuwa akimuombea mara zote, ikiwa ni pamoja na kipindi alichokuwa mwanachama wa CHADEMA.
“Mwanangu alibezwa na hata kuonekana kuwa si lolote katika chama awali na kupewa majina mbalimbali, aliambiwa hata akitoka CHADEMA hatakuwa na athari zozote, lakini sasa kila Mtanzania anashuhudia kinachoendelea”. 

“ACT ni chama kidogo lakini kinaongoza mitaa na vijiji na kimefanikiwa kuwa na wanachama wengi, sasa najiuliza hivi hawa waliokuwa wanasema hana madhara, inakuwaje wanamkebehi Na hata kumuhofia?. 

Anasema aliumia baada ya mwanaye kufukuzwa CHADEMA lakini sasa dunia yote inashuhudia hali halisi ilivyo kutokana na maono ya kijana wake.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.