Wednesday, March 25, 2015

Anonymous

WASTARA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU SKENDO YA KUTOKA NA ALIYEKUA BWANA WA WOLPER

Kupitia ukurasa wake wa ‘fesibuku’ Wastara amendika;
“Kalamu ya muandishi imegeuka kuwa fimbo ya wanyonge tofauti na miaka ya nyuma,waandishi wanakula mishahara mara mbili wa kituo anachofanyia kazi na wa mtu anaempa habari,hivyo kuandika anachoambiwa sio anachokiona 

Pesa inatumika kupotosha ukweli na ukweli ndio uongo waleo,nimeamini maneno yangekuwa sumu ningeshakufa zamani sana lakini kwakua mdomo nyumba ya maneno bado niko hai
Tupendane tushikamane na tuishi kwa usawa usipende kuonea unachoambiwa ongea unachokijua,sio pesa ikufanye kuharibu image nzima ya mtu kwanza kwa pesa gani? 

Allah ndio amenitengeneza na ndio atakaenichukua akiamu na ndio mwenye uwezo wa kunishusha na kunipandisha lakini sio wewe tuliokutana duniani”.- wastara alimaliza.
Hivi juzi kati Watara alidaiwa kutoka na alikuwa bwana wa Jaqline Wolper anaefahamika kwa jina la  Mark Edi ambae ni mfanya biashara wa mavazi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.