Wednesday, April 1, 2015

Anonymous

MAMIA WAJITOKEZA KUMUONA LOWASSA BAADA YA KUDANGANYWA UJIO WAKE MKOANI IRINGA



MAMIA ya wakazi wa mji wa Iringa mapema asubuhi ya leo ‘SIKU YA WAJINGA DUNIANI’ walijitokeza katika uwanja wa Mwembetogwa, mjini hapa kumlaki na kumsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.

Taarifa ya kiongozi huyo mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli zilisambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya simu na baadaye kutangazwa na vyombo vya habari kadhaa za mjini hapa.

Wakati watu wakiendelea kukusanyika katika uwanja huo huku kukiwa hakuna maandalizi yoyote yaliyoashiria ujio wa kiongozi huyo, vyombo hivyo vya habari viliomba radhi kwa kuwakumbusha wananchi waliokuwa wakiendelea kufurika katika uwanja huo kwamba leo ni siku ya WAJINGA.

Mtandao huu ulishuhudia waliokuwepo uwanjani hapo wakianza kutawanyika mmoja mmoja na kimakundi kama walivyojitokeza.

SIKU YA WAJINGA iliitwa ivyo baada ya Steve April aliyezaliwa April 1, 1579 kwenye familia ya kitajiri huko America kufanya biashara zaidi ya 105 kwenye maisha yake yote lakini alibaki masikini.

Hiyo ilifanya kila mtu amuite MJINGA.Baadae wakamuita Baba wa Wajinga Duniani.
Alikua akisoma na kuamini stori za kijinga kama hii unayoisoma sasa ivi.
Nakutakia kheri ya Mwezi mpya na siku njema ya wajinga duniani.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.