Watu wawili wamekufa katika manispaa ya Songea baada ya kupata ajali ya pikipiki,waliofariki ni dereva wa pikipiki na abiria wake ambao wamepata ajali eneo la Ruhuwiko baada ya kuchomekewa na pick up.
Mashuhuda wamesema siku ya leo watu wengi wamelazimika kutumia usafiri wa pikipiki baada ya daladala kugoma kufuatia mgomo wa wafanyabiashara, wameendelea kusema ajali hiyo yawezekana isingetokea endapo kungekuwa na usafiri wa daladala yawezekana binti huyo asingepanda pikipiki.




Note: Only a member of this blog may post a comment.