Friday, February 13, 2015

Anonymous

ZILIPENDWA WA DIAMOND, PENNY AFUNGUKA KUHUSU MCHUMBA NA NDOA YAKE!

Na Hamida Hassan/Ijumaa 
Mtangazaji aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul, ‘Diamond’,  Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kusema kuwa anashukuru amepata mchumba ila suala la ndoa siyo la leo wala kesho.
Mtangazaji aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul, ‘Diamond’,  Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Akipiga stori na Ijumaa juzikati, Penny alisema wengi wamekuwa wakitaka kusikia suala la yeye kuolewa baada ya kubainika ana mchumba lakini mwenyewe anasema hajafikiria hilo la kuitwa mke kwa sasa. 

“Kwenye hilo la kufunga ndoa naweza kusema bado niponipo sana, yapo mambo yangu ambayo lazima niyakamilishe kabla ya kuolewa, ndoa si mchezo, kujipanga ni muhimu,” alisema Penny.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA!   

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.