Usiku wa April 22 2016 winga wa Azam FC mtanzania Farid Musa aliondoka Tanzania na kwenda Tunisia na baadae alienda kufanya majaribio Hispania katika klabu ya Tenerife inayoshiriki Ligi Kuu daraja la pili Hispania.
Farid alifanya majaribio na kufanikiwa kufuzu na baadae kurudi Tanzania akiwa anasubiria kwenda kujiunga rasmi na klabu hiyo, hadi sasa Farid yupo Dar es Salaam kitu ambacho kimemgusa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta.
“Asalam
aleikhum? Niliposikia farid anaenda Spain kwa majaribio nilipata furaha
sana kwa Kuwa niliamini kwa kipaji alichonacho asingeweshindwa
majaribio ktk club ile aliyokuwa anakwenda na ndivyo ilivyokuwa furaha
iliongezeka baada ya kusikia azam wamemruhusu kwenda kuanza Maisha ayo
mapya ya soka ulaya” >>> Samatta
“kwa
nini niwe na furaha kwa sababu naamini maendeleo ya timu yetu ya taifa
yatapiga hatua kwa haraka tukiwa na wachezaj wengi wanaocheza soka la
kulipwa nje ya tanzania,(imani yangu)lakini kadri siku zinavyokwenda
nimekuwa simsikii farid akiwa ktk club yake mpya na habari zilizopo ni
Kuwa bado yuko tanzania,je ni kwa nini bado yupo tanzania wakati kila
kitu kilishakwisha nani ana jibu la swali hili? Tafadhari?kuna nini
nyuma ya pazia” >> Samatta
Note: Only a member of this blog may post a comment.