Siku ya
kwanza ya May 2016 jina la Mzee Majuto limetajwa tena kwenye vichwa vya
habari kuhusu kuacha kwake kuigiza, kama utakumbuka aliwahi kuongea na
Millard Ayo mwaka 2014 na kusema angestaafu kuigiza mwaka 2015 lakini
hakustaafu, akaendelea na movie zake.
Kauli yake mpya leo May 1 2016 kupitia Instagram ya CloudsFM kuna maelezo yafuatayo >>> ‘Gwiji
la sanaa ya maigizo nchini Amri Athmani aka Mzee Majuto ametangaza
rasmi kustaafu kuigiza na kutumia muda wake kumtumikia mola wake. Majuto
amekuwa akifanya sanaa hii ya maigizo kwa muda mrefu na alianza kupata
umaarufu mwanzoni mwa miaka ya 90’
Note: Only a member of this blog may post a comment.