Tafiti nyingi kuhusu wanaume wafupi, zinasema wanaume wafupi wanamapenzi ya kweli na ya dhati kuliko wanaume warefu, kitu ambacho siwezi kubisha kwa sababu wanawake wengi hawapendi kutoka na wanaume wafupi hivyo inawachukua muda kupata mwenza na lazima wawapende na wawape mapenzi ya kweli wanawake zao ili wasiwaache kwa sababu wanawake wengi wanapenda mwanaume warefu na wengi wanamvuto kuliko wafupi.
Wanawake wengi wanapenda kutoka na wanaume ambao wamewazidi urefu hata kidogo, kuliko kuwa na mwanaume ambaye ni mfupi kuliko wao, wengi wanasema hii inaleta picha mbaya au muonekano mbaya wakiwa wanaongozana wanaita (Not Matching), pia zipo sifa nyingine za wanaume wafupi ambazo hugeuka kero kwa wanawake walio wengi kama vile :-
Wivu
Inasemekana wanaume wafupi wanawivu wa kupindukia na sio kama wanaume warefu hawana wivu la hasha ila wao wana wivu unaopitiliza kiasi cha kukera kwani wivu ukizidi sana ni kero katika mapenzi.
Sifa
Wanaume wengi wafupi wana sifa na majigambo ambayo hugeuka kero kwa wapenzi wao kwa vile hutaka kuonekana kama wapo eneo fulani kila mtu atambuwe uwepo wao ingawa pia wanasifa moja ya kuwa na uchechi.
Gubu
Hapa sasa ukichanganya na wivu ni balaa maana mwanaume mwenye gubu ni zaidi ya mwanamke muongeaji, Gubu ni ile hali ya kukosoa kila kitu, kila kitu kibaya, yeye haridhiki na chochote wakati mwingine atakuona huwezi chochote akiwa karibu atatafuta sababu ya kuongea tu.
Wanajidai Wanajua kila kitu ( Much Know)
Much knows, hapa bwana unakutana na mtu kila kitu anajua yeye, ni kero kwa sababu akiwa mbele za watu atataka kila mtu ajue anajua nini kama inaongelewa siasa, mpira au mapenzi yeye fundi wa kila kitu, kitu ambacho kiukweli kinakera na kuudhi wakati mwingine.
Muonekano/ Mvuto
Wanawake wengi wanasema wanaume wafupi hawana mvuto kama wanaume warefu na hiyo ni moja ya sababu ya wao kutotaka kutoka na wanaume wafupi katika mahusiano japokuwa sio wanaume wote wafupi hawana mvuto.
Japokuwa inasemekana siku hizi hakuna anaeangalia urefu ama uzuri wa mwanaume bali asilimia kubwa ya wanawake wanangalia mfuko yaani pesa, shekeli, mshiko ama madini ingawa hayo ni maneno ya mitaani watu wanaongea. Mimi binafsi sina hakika kama yanayozungumzwa yana uhalisia wowote.

Note: Only a member of this blog may post a comment.