Thursday, April 14, 2016

Anonymous

PUNYETO! ATHARI ZA KUJICHUA NYETI

Karibu tena Mpendwa Mwanafamilia ya www.kandiliyetu.com katika uwanja wa mahaba kwani kupitia Uwanja huu tunapata kujifunza vipya kila siku katika kuboresha MAHUSIANO kama kawaida leo tunapata shule nyingine ambayo namatumaini inaendelea kukujenga kiakili na kimahusiano.

Neno PUNYETO sio geni katika masikio yako lakini leo naomba niongelee suluhisho au jinsi gani mtu anaweza kuacha punyeto kabisa Punyeto ni tatizo la tabia na linaweza kudhibitika kabisa kama matatizo mengine yeyote basi ilikuacha tabia hiyo hebu ungana nami nikuelekeze nini cha kuzingatia.

FANYA YAFUATAYO.
Acha kuangalia video za Ngono: Video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayo iona utataka uka ipigie punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako, weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga kwani bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.


Epuka kukaa nyumbani peke yako, mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine.

Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata hasa madogo madogo kama uchovu mkubwa,kuumwa kichwa na kusahau sana hii itakupa moyo wa kuendelea kutopiga punyeto.

Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho, siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena,hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema ivoivo, kama unaacha acha mara moja.

Tafuta mpenzi kama huna kabisa: ukiwa na mpenzi madhara ya punyeto kama kupungukiwa nguvu za kiume yatakufanya uache kabisa kwani ukiendelea utaaibika siku moja pale uume utakaposhindwa kusimama kabisa mkiwa faragha chumbani na pia utapata nafasi ya kushiriki tendo la ndoa hivyo kuacha kabisa punyeto.

Pia unaweza kumshirkisha mwenzi wako tatizo lako ili akusaidie kuacha.
Anza mazoezi na jishughulishe na mambo mengine:Hii itakufanya uwe bize na mambo mengine na utumie mda wako mwingi huko, pia mazoezi ya jioni yatakufanya uchoke na kushindwa kufikiria kupiga punyeto wakati wa kwenda kulala.


Uzoefu unaonyesha, mtu anayepiga punyeto, hata kama ameathiriwa na tatizo la punyeto kwa kiwango gani, endapo atafanikiwa kutopiga punyeto kwa muda wa siku arobaini mfululizo, mtu huyo hatopiga tena punyeto katika siku zote za maisha yake kwani tayari mtu huyo atakuwa amerudia katika hali yake ya kuto kuwa addicted tena na upigaji punyeto, na atalichukia kabisa hata jina la tendo hilo achilia mbali tendo lenyewe.

Pia ieleweke kuwa sio rahisi kwa mtu aliyekuwa addicted na punyeto kustahimili kujizuia kupiga punyeto kwa muda wa siku arobaini mfululizo, Anaweza kujizuia kupiga punyeto kwa siku mbili lakini baada ya hapo ataendelea tena na mchezo wake.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.