Friday, April 8, 2016

Anonymous

Ni Miaka Minne Toka Kifo Cha KANUMBA, Haya ni Mahojiano na Mama Yake

Bado kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa msanii wa filamu za maigizo Tanzania Steven Charles Kanumba kipo akilini mwa watanzania wengi hususani familia yake ambayo kila ifikapo April 7 hufanya ibada kwa ajili ya kumkumbuka staa huyo.

April 7 2016 Kanumba ametimiza miaka minne toka afariki dunia April 7 2012 baada ya kuanguka nyumbani kwake Sinza Dar es Salaam, April 7 2016 familia, ndugu, jamaa na marafiki walikusanyika kufanya ibada ya pamoja katika kaburi la Kanumba Kinondoni Dar es Salaam, baada ya hapo Ayo TV ilimpata mama Kanumba katika exclusive interview, Bi Flora Mtegoa.

“Kiukweli nimefurahishwa kumuona mama Lulu makaburini na kuweka shada la maua katika kaburi la Kanumba nampongeza sana kwa ujasili licha ya kuwepo kwa maneno maneno, kuhusu kampuni ya Kanumba bado ipo na inafanya kazi ila ofisi tumehamishia nyumbani kutokana na kodi kuwa kubwa” >>> Flora Mtegoa
Unaweza kutazama interview yote ya mama Kanumba hapa

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.