MAYASA MARIWATA
LEJENDARI wa Muziki wa Bongo Fleva,
Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ hivi karibuni katika uzinduzi wa video ya
wimbo wake mpya wa Ndi Ndi Ndi alizua gumzo kutokana na gauni alilokuwa
amevaa kuwa na mpasuo mkubwa na kuacha sehemu
mwili wake wazi.
Ishu hiyo iliyochukua nafasi pande za Samaki Samaki, Masaki jijini Dar, mastaa kibao walihudhuria wakiwemo Martin Kadinda na Raheem Nanji ‘Bob Junior’ na muda mwingi bi’shosti huyo alionekana akiwatoa udenda wanaume wakware na kuzua gumzo.

“Duhh! Naona leo katuamulia kututega, maana ule mpasuo kweli ni Jide mpya,” alisikika mmoja wa mashabiki.
Jide alipofuatwa na kuulizwa kuhusiana na ishu hiyo aligoma kuzungumza na kumtaka mwandishi aonane na msemaji wake ili apange naye ‘appointment’ jambo ambalo liligonga mwamba.

Note: Only a member of this blog may post a comment.