Tuesday, April 19, 2016

Anonymous

Iggy Azaleo Akana Kumwagana na Nick Young

Mwanamuziki nyota wa Marekani, Iggy Azalea akiwa na mpenzi wake Nick Young.
MWANAMUZIKInyota wa Marekani, Iggy Azalea, amekana kwamba ameachana na mpenzi wake ambaye ni nyota wa mchezo wa kikapu (basketall) wa Los Angeles Lakers, Nick Young.
Kauli hiyo ameitoa ili kuondoa minong’ono iliyokuwepo kwamba wamemwagana kutokana na madai kwamba Nick alikuwa anamsaliti kimwana huyo kwa kuwa na michepuko kadhaa.

Katika kurasa zake za mtandao, mrembo huyo aliandika: Iggy Azalea, 25, na Nick Young, 30, hawatengani! Tumekuwa tukijiuliza iwapo bado wanaendeleza uhusiano wao baada ya kutolewa video iliyofichua kwamba Nick amekuwa akimsaliti mwenzake. Hivi sasa anatoboa ukweli na kumaliza majadiliano: Mapenzi yao bado yanaendelea.

Aliendelea kusema: “Kwa ajili ya kuweka kumbukumbu vyema, sijaachana na Nick. Tuko pamoja, na naomba tuachwe kufanya mambo yetu kwa faragha!
“Kila mara huwa ninajibu maswali kwa kwa uadilifu,” aliendelea kuandika. “Lakini kazi yangu ni kupromoti muziki wangu, si uhusiano wangu na watu wengine.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.