Kijana Karimu Said ‘Anti Karim’ akitoa ushuhuda redioni.
STORI: Dustan Shekidele, Ijumaa Wikienda
Morogoro: My confession! Katika hali
isiyo ya kawaida, kijana Karimu Said (25) almaarufu Anti Karimu
aliyekiri kufanya biashara haramu ya kuuza mwili (ushoga), ameangua
kilio redioni wakati akiutangazia umma wa Watanzania kuachana na dhambi
hiyo aliyodumu nayo kwa miaka saba.
Anti Karim akiendelea kufunguka.
Ilikuwa Alhamisi iliyopita, Karimu
alifika katika ofisi ndogo za gazeti hili za mkoani hapa na baadaye
alitinga kwenye Kipindi cha Mcharuko wa Pwani cha Radio Planet FM
kinachoendeshwa na mtangazaji mahiri, Warda Makongwa akishirikiana na
Farham Abraham.
Lengo la Karimu lilikuwa ni kutubu dhambi yake hiyo sambamba na kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu na Watanzania kwa jumla.
Lengo la Karimu lilikuwa ni kutubu dhambi yake hiyo sambamba na kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu na Watanzania kwa jumla.
Akiwa hewani laivu kwenye kipindi hicho
na watangazaji hao na mwandishi wetu, Karimu alisimulia kilichomwingiza
kwenye ushoga kuwa ni umaskini uliotokana na vifo vya wazazi wake.
“Nikiwa hapo, bosi wangu wa kike na wanaye walikwenda likizo kijijini, mimi nilibaki na bosi wa kiume.
“Siku moja huyo mwanaume alinirubuni akanipeleka beach (ufukweni) na baadaye Mlimani City ambako alinilazimisha kunywa pombe.
“Siku moja huyo mwanaume alinirubuni akanipeleka beach (ufukweni) na baadaye Mlimani City ambako alinilazimisha kunywa pombe.
“Tuliporudi nyumbani aliniingilia, tangu
hapo kila siku akawa akinifanyia hivyo. Mkewe aliporudi alinikanya
nisimwambie, nikajikuta namuonea wivu huyo mwanaume hata akiwa na mkewe.
“Hali hiyo ilisababisha mkewe kujua na kunitimua,” alisema Karimu.
Alisema kuwa baada ya kutimuliwa alirejea kwao Morogoro na kuendelea na ushoga akijiuza kwenye madanguro yaliyopo ltingi na Kahumba mjini hapa.
Alisema kuwa baada ya kutimuliwa alirejea kwao Morogoro na kuendelea na ushoga akijiuza kwenye madanguro yaliyopo ltingi na Kahumba mjini hapa.
Alipoulizwa wateja wake wakubwa ni watu gani, Karimu alifunguka kuwa ni waume za watu wakiwemo baadhi ya vigogo wa serikali.
Mwandishi wetu alipomtaka kuelezea
changamoto alizokumbana nazo, alifunguka huku akiangua kilio studio:
“Changamoto ni nyingi zikiwemo za kupigwa, kupata bwana akakulipa elfu
arobaini lakini ukifika geto kwake, ukishamhudumia, anakugeuka na
kukunyang’anya fedha.
“Nimeyatafakari matukio yote hayo, ndipo
nikaungana na rafiki yangu aliyenipeleka kanisani ambako niliombewa
hadi nikaanguka, nikapoteza fahamu, nilipozinduka nikajiona niko kwenye
ulimwengu mwingine na kujutia dhambi hiyo ya ushonga, hivyo naomba Mungu
na Watanzania wanisamehe,” alisema Karimu huku akilia.
Note: Only a member of this blog may post a comment.