Mfungaji wa bao la kwanza la Simba, Danny Lyanga.
Mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza akidhibitiwa na mabeki wa Mbeya City.
MABAO mawili yaliyofungwa na Danny Lyanga na Ibrahim
Ajib katika dakika ya 75 na 90 yameipa Simba ushindi wa mabao 2-0 dhidi
ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Danny Lyanga
Simba imepata ushindi katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambapo sasa
imeshika usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 48 ikiizidi Yanga
ambayo ina pointi 47 sawa na Azam inayoshika nafasi ya tatu.
Ushindi huo ulisababisha shangwe nyingi kwa mashabiki wa Simba ambao
waliondoka uwanjani hapo wakiwa na furaha huku wakishangilia barabarani.
Mara baada ya mchezo huo, Kocha wa Simba, Jackson Mayanja alisema
anashukuru mashabiki wa timu yake kwa kuendelea kuiunga mkono timu yao
huku akipongeza wachezaji wake kwa kuifunga Mbeya City kwa mara ya
kwanza katika uwanja huo.
Upande wa Mbeya Ciy, Kinnah Phiri alisema kilichotokea ni timu yake
kukosa bahati tu lakini vijana wake walicheza vizuri. Kingine alisema
wachezaji wake walikuwa wakipata nafasi ya kupiga mashuti lakini
hawakufanya hivyo, ameahidi kwenda kulifanyia kazi suala hilo.
Kikosi cha Simba:
- Vincent Angban
- Emiry Nimubona
- Mohamed Hussein ‘Tshabalala’
- Novaty Lufunga
- Juuko Murshid
- Justice Majabvi
- Mwinyi Kazimoto
- Jonas Mkude
- Hamis Kiiza
- Ibrahim Ajib
- Brian Majwega
Kikosi cha Mbeya City
- Hannington Kalyesebula
- Hassan Mwasapili
- Abubakar Shaban
- Tumba Sued
- Haruna Shamte
- Kenny Ally
- Raphael Alpha
- Haruna Moshi ‘Boban’
- Geofrey Mlawa
- Joseph Mahundi
- Ditram Nchimbi
Note: Only a member of this blog may post a comment.