Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba.
Sakata la Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na
Muungano), January Makamba na Mdogo wake Mwamvita kudaiwa kupokea rushwa
kutoka kwa raia wa Italia, Vincenzo Cozzolino ili wamsaidie kupata
zabuni ya ujenzi limechukua sura mpya.
Sauti na jumbe mbalimbali zilizosambazwa na kuwekwa kwenye mtandao na
mmiliki wa tovuti ya U-Turn, Mange Kimambi, raia wa Tanzania aishie
Marekani, zinaonesha mazungumzo kati ya watatu hao, mwaka 2011. Jana,
Mwamvita na Makamba walikiri kuwa sauti hizo ni za kweli.
Msikilize Mhe. January Makamba akifunguka kuhusu sakata hilo hapa chini:
Muitaliano
huyo ambaye anadaiwa kumpa Mange Kimambe ushahidi wote wa mawasiliano
kati yake na Ndugu hao, amejitokeza na kuwasafisha akidai kuwa hakuwahi
kuwapa rushwa wala kuhusiana na January kibiashara.
Cozzolino ameandika ujumbe akidai kuwa ingawa yeye na Mwamvita
walikuwa na uhusiano wa mapenzi mwaka 2011 na baadaye kujiingiza katika
biashara binafsi ambayo ilipelekea kugombana kwao, hawakumhusisha
January kwa aina yoyote katika biashara yao.
“Sikuwahi kumuomba [January] kunisaidia katika biashara zangu.
Sikuwahi kumpa fedha. Mara chache nilizokutana naye ilikuwa ni
mazungumzo ya kawaida ya kijamii. Nilikuwa na uhusiano na Mwamvita.
Uhusiano wetu ulikuwa bomba mwanzoni lakini ukawa na mwisho mbaya,”
ameandika Cozzolino.
Mwamvita Makamba.
Awali, sauti ya January na mwandishi wa habari iliyosambazwa, January
anasikika akieleza kuwa aliwahi kukutana mara moja Dubai na Muitaliano
huyo na kwamba alitambulishwa kama mpenzi wa dada yake.
Alisema baadaye dada yake alimwambia wameanza kufanya biashara ya
kahawa na Muitaliano huyo na baadae biashara hiyo kufa huku ikiwaacha
katika mzozo.
Kwa mujibu wa Kamambe, Muitaliano aliyekuwa ameweka nusu ya mtaji
ambayo ni dola milioni 50, alianza kudai kiasi hicho cha fedha na sio
vinginevyo.
Ufuatao ni ujumbe alioandika Vincenzo Cozzolino ukionyesha kuwa January Makamba hausiki na sakata lao:
Alisema kuwa awali, Muitaliano huyo alikuwa anajaribu kumshawishi
Mwamvita amkutanishe na viongozi wakubwa wa serikali ikiwa ni pamoja na
Katibu Mkuu.
Hata hivyo, Mange Kimambe ambaye ndiye anayeeleza kuwa na nyaraka
zote za ushahidi aliokabidhiwa na Muitaliano huyo na kwamba hivi sasa
Muitaliano amelipwa na kukubaliana kumsafisha Mbunge huyo wa Bumbuli.
Mange amesisitiza kuwa ana ushahidi wote wa January na dada yake
kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara huyo na yuko tayari kuwakabidhi
Takukuru.
Note: Only a member of this blog may post a comment.