Thursday, March 10, 2016

Anonymous

Picha: Mapokezi ya LULU Michael Tanzania yawashtua Afrika Magharibi

Mapokezi ya Elizabeth ‘Lulu’ Michael wiki hii yameishtua Afrika Magharibi.
Lulu alishinda tuzo ya filamu bora ya Afrika Mashariki kwenye tuzo za Africa Magic Viewers Choice, AMVCA 2016 zilizotolewa Jumamosi nchini Nigeria. Muigizaji huyo alipokelewa kishujaa na mashabiki alipowasili Jumanne hii akitokea Lagos.

Mapokezi hayo yametuma ujumbe Nigeria ambako website maarufu za huko zimempa mashavu.

Blog namba moja wa burudani nchini humo, The Net, umeandika habari yenye kichwa kisemacho: Tanzanian actress gets heroic welcome after ‘winning big’ at AMVCA.
Blog nyingine iliyoandika ni The Nigerian Bulletin.

Kwa muda mrefu Tanzania kwa nchi za magharibi mwa Afrika imekuwa ikijulikana kwa muziki wa Bongo Flava zaidi na hivyo ni kitu cha kutia moyo kuona wasanii wa filamu wanaanza kupata majina huko pia.

Hiyo inamaanisha kuwa ushindi wa Lulu unaweza kumsaidia kujitanua zaidi nje ya Tanzania na huenda kuanza kufanya filamu na wasanii wa huko. Lulu ana kila sifa ya kuwa msanii wa kimataifa.
Nampongeza kwa mara nyingine kwa ushindi huo
-Bongo5

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.