Friday, March 18, 2016

Anonymous

NYAMAYAO na Simulizi ya Kuchomwa Kisu!


IMG_0536Happiness Stanslaus  ‘Nyamayao’.
Wiki hii tunaye msanii mkongwe kwenye tasnia ya uigizaji Bongo. Huyu anakwenda kwa jina la Happiness Stanslaus ambaye wengi tunamfahamu kwa jina la ‘Nyamayao’. Mwandishi Wetu Hamida Hassan alikutana naye na kumbana maswali 10. Je, unataka kujua aliulizwa nini na akajibu vipi? Fuatilia hapa chini…
Ijumaa: Umekuwepo kwenye fani kwa muda mrefu, unaionaje sanaa ukilinganisha zamani na sasa?
Nyamayao: Zamani ilikuwa ili uwe msanii lazima upitie kwenye vikundi ukapikwe lakini sasa hivi yeyote anaweza kuwa msanii bila hata mafunzo yoyote.

Ijumaa: Wewe ni mama na una watoto wa kike, unawalinda vipi wasiharibiwe na huu utandawazi?
Nyamayao: Malezi ni magumu kiukweli, inabidi wazazi tuwe wazi sana, tuwe marafiki kwa watoto wetu ili waweze kutueleza kila kitu wanachokutana nacho huko. Zamani ilikuwa ukivunja ungo unaambiwa usicheze na wavulana bila kuelezwa chochote kwa undani, kwa sasa ni ngumu inabidi kuwa wazi kwenye kila kitu.

Ijumaa: Sasa hivi wasanii hasa wa kike wamegeuza kwenye filamu kama sehemu ya kujiuza, unalizungumziaje hilo?
Nyamayao: Mimi naona ni hulka ya mtu, ukiwa na tabia mbaya hata sanaa isingekuwepo bado ungefanya ufuska wako.
Ijumaa: Watu wanatamani kumuona yule Nyamayao wa zamani, atarudi kweli?
Nyamayao: Siyo atarudi, amesharudi na sasa nimedhamiria kuwaonesha watu kuwa kwenye sanaa siyo sehemu ya kuuza sura ni kazi tu.

Ijumaa: Ni wasanii gani ambao unaona sanaa wanaimudu na wewe unawakubali?
Nyamayao: Kiukweli ni wengi ila kwa kuwataja wachache ni Kemmy, Thea, Riyama, Bi Staa, Swebe na Monalisa.
Ijumaa: Umesomea Uandishi wa Habari na kuna wakati ulikuwa ukiifanya kazi hii ni kwa nini uliacha?
Nyamayao: Sijaiacha ila sifanyi kazi kwenye media, naandika hadithi zinazotumika kwenye filamu na tamthiliya.
Ijumaa: Ukiwa nyumbani unapenda kufanya kazi gani?
Nyamayao: Ukiacha zile kazi za mwanamke kama kupika, kufanya usafi na nyinginezo, napenda kuandika hadithi zangu.
Ijumaa: Ni chakula gani unachopendelea kupika?
Nyamayao: Mimi bwana napendelea sana ugali kwa dagaa na matembele.

Ijumaa: Katika filamu ulizowahi kucheza ni filamu gani ambayo unakiri uliitendea haki na huwezi kuisahau katika maisha yako?
Nyamayao: Kuna filamu inaitwa Prisoner ya Marehemu Chaiba Kombo, katika hiyo filamu kuna scene nilitakiwa kuchomwa kisu, zikaandaliwa sehemu ambazo nitachomwa kisu nisiumie. Bahati mbaya yule aliyetakiwa kuigiza hiyo scene akanichoma kikwelikweli kwenye mkono.
Ijumaa: Naona wewe unacheza sana Tamthiliya, je ni ipi unaipenda na kipengele kilichowahi kukufurahisha ni kipi?
Nyamayao: Kwenye Tamthiliya ya Fukuto nilipenda sana kipengele nilichochezwa ngoma wakati naenda kuolewa na Mzee Pwagu. Kwa sasa kwenye Tamthiliya ya Usaliti nilipenda pale nilipomuibia bwana pesa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.