Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar bado yupo kwenye headlines za ukwepaji kodi, kama ambavyo zilivyokuwa zinawakabili mastaa wenzake wa FC Barcelona Lionel Messi na Javier Mascherano.
Neymar ameripotiwa
kukutwa na hatia ya ukwepaji kodi wa euro milioni 56.4, kutokana na
makosa mawili ya ukwepaji wakati wa uhamisho wake kutoka Santos kujiunga na FC Barcelona na mkataba wake Nike, makosa hayo yamefanyika kupitia kampuni zake za (Neymar Sport e Marketing, N & N Consultoria, N & N Administracao de Bens) kati 2012 na 2014.
Kwa mwaka 2016 pekee Neymar anakuwa mchezaji wa pili ya FC Barcelona kukutwa na kosa hilo, aliwahi kuhukumiwa mwaka mmoja Javier Mascherano ila adhabu yake ikabadilishwa na kuwa faini. Sheria za Hispania zinaeleza kuwa mtu akikutwa na hatia ya ukwepaji kodi anaweza badili kifungo na kulipa fedha.
Kutokana na makosa hayo ya Neymar aliyoyafanya,
amepewa adhabu ya kulipa faini ya euro milioni 45.9 pamoja na kulipa
kiasi alichokwepa kulipa kama kodi, kwa sheria ya Hispania kama Neymar atashindwa kulipa faini hiyo, huenda akakumbana na kifungo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.