Ishu hiyo ambayo inawakumba wasanii wengi wasio na magari, lakini katika uchunguzi wa gazeti hili wiki iliyopita, lilifanikiwa kuwanasa wasanii wawili, Isabella Francis ‘Vai wa Ukweli’ aliyenaswa maeneo ya Kinondoni jijini Dar na Coletha Raymond ‘Koleta’ aliyenaswa Magomeni, pia Dar.
Hawa walinaswa na mashushushu wetu kwa nyakati tofauti wakihangaika kubadilisha usafiri wa Bajaj kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwenye mizunguko yao pasipo kujali gharama.
Paparazi wetu alipombananisha Koleta alisema: “Ni kweli natumia fedha nyingi kwenye usafiri wa Bajaj kwa sababu ni wa haraka tofauti na kukodi teksi. Na hakuna kitu nisichokipenda kama kupanda daladala.
Vai wa ukweli naye akitumia usafiri huo.
“Siyo kwa sababu ya kujulikana ndo’ maana sipendi kupanda daladala. Kingine kinachoniboa ni jinsi watu wanavyobanana kwenye huo usafiri, matumizi yangu ya siku kwenye Bajaj si chini ya shilingi elfu 50 japokuwa ni nyingi lakini pesa ukiwa nayo unatumia bwana.” Kwa upande wake, Vai wa Ukweli alisema: “Kusema kweli usafiri wa Bajaj unaturudisha wasanii nyuma kimaisha, lakini suala la kupanda daladala nalo lina ugumu wake. Umaarufu tabu sana lazima uishi maisha ambayo mashabiki wako wanayatarajia. Mimi matumizi yangu ya Bajaj kwa siku si chini ya shilingi elfu 60.”
Baadhi ya wasanii wengine ambao wamekuwa wakishuhudiwa kwenye kupanda Bajaj ni Gift Stanford ‘Gigy Money’, Khadija Maige ‘Kadja Nito’, Asha Salum ‘Kidoa’, Moshi Katemi ‘Mo Music’ bila kumsahau Pamela Daffah ‘Pam D’ ambaye paparazi wetu aliwahi kumsikia akilalamika jinsi usafiri huo unavyomrudisha nyuma kimaisha kiasi cha kumkwamisha mpango wake wa kununua gari.
Imeandaliwa: Hamida Hassan, Mayasa Mariwata na Gladness Mallya
Note: Only a member of this blog may post a comment.