Tuesday, March 8, 2016

Anonymous

Mapacha Waliokufa Kwa Uzembe Hospitali ya Nyamagana… Simulizi Inauma Sana!

Butimba (2)Wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo.
Stori: Idd Mumba, UWAZI
Mwanza: Simulizi inayouma na kusikitisha imetolewa juu ya uzembe uliosababisha vifo vya mapacha wawili katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, Mwanza, vilivyotokea wiki iliyopita baada ya mama mmoja kulazimika kujifungulia watoto hao kwenye beseni.
Mama wa watoto hao mapacha, Susan John aliliambia gazeti hili kuwa mapema aliwaambia manesi juu ya siku zake za kujifungua kukaribia, lakini manesi hao walimjibu jeuri na dharau, wakimwambia muda wake wa kujifungua bado haujafika na wala asiwafundishe kazi.
1. MAGU
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
“Mimi niliwaeleza manesi hali yangu kuwa najisikia vibaya, lakini walinijibu vibaya na kutoa lugha ya matusi huku wakisema siku bado wakati mwili wangu ndiyo nauona mabadiliko yake, niliamua kunyamaza kimya maana kupata msaada ilikuwa shida, wakati nikisubiri nilijihisi kupatwa na haja ndogo ikabidi niende msalani, nilikojoa kidogo tu, mara nikaona mtoto wa kwanza anatoka akiwa ametanguliza makalio, kulikuwa na beseni jirani nililivuta na kutegesha ndipo nikazaa watoto wangu mapacha bila msaada wowote.

“Ndugu niliokuwa nao walienda kuwaita manesi, lakini hawakufika mapema mpaka watoto wote wakafariki japo niliwazaa wakiwa hai, niliamini nimejikomboa, sitasahau tukio hili..(kilio)” alisema Suzan.
Mashuhuda wa tukio hilo walimtaja muuguzi mmoja (jina tunalo) kutamka maneno mabaya kwa mama huyo huku akidai hakuna mtu wa kumfanya chochote.

Kufuatia tukio hilo la kusikitisha, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo amewasimamisha kazi madaktari wawili na wauguzi watatu kupisha uchunguzi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa endapo itathibitika kuwepo kwa uzembe uliosababisha vifo hivyo.

Madaktari waliosimamishwa kupisha uchunguzi huo ni Dk. Nolyne Magesa na Dk. Emilian Mvungi huku wauguzi wakiwa ni Ngusa Masanja, Vivian Moshi na Mariam Mkankule.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.