Na Mwandish wetu, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Wakati ajali
mbaya iliyohusisha magari matatu ikiwa bado ndani ya vichwa vya watu
jijini Dar es Salaam, baadhi ya mashuhuda wanaelezea maajabu
yaliyoambatana na tukio hilo lililotokea Jumatano, likihusisha daladala
aina ya Toyota DCM linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto na
Ubungo.
Maofisa wa Polisi wakiwa eneo la tukio.
Ajali hiyo ilitokea baada ya daladala
yenye namba za usajili T 629 CTT ikiwa na abiria, kugongwa kwa nyuma na
lori aina ya Scania lililokuwa limebeba mchanga, lenye namba za usajili T
447 DBH na kuifanya daladala hiyo kupoteza mwelekeo na hivyo kuhama
kutoka upande wake hadi wa pili ambako liligongana na Scania lingine
lenye namba za usajili T 109 DDX, lililokuwa katika mwendo mkali na
kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi 25.
“Nilikuwa
ndiyo naingia barabarani ili niende kupanda gari kituoni (Matumbi),
nikasikia kishindo kikubwa upande ule wa pili, nilipoangalia vizuri
ndipo nikaiona daladala inahamia upande huu, wakati huo lori la ng’ombe
nalo lilikuwa linakuja kwa kasi sana. Katika taa kali za gari, nikawaona
paka wawili wakiwa katikati ya barabara,” anasema Korongo Japhet,
aliyejitambulisha kuwa ni mkazi wa Kigogo Dampo.
Alisema wakati akitafakari
kitakachotokea, mara alisikia kishindo kikubwa kilichofuatiwa na kelele
nyingi kutoka kwa wasafiri na watu waliokuwa kituoni wakisubiri usafiri.
“Mimi nililiona lile DCM likipanda ukuta
wa barabara kuhamia upande wa pili, kitu cha ajabu ninachokumbuka kuona
ni njiwa wawili weupe wakiruka juu ya ile daladala, lakini sekunde
chache baadaye sikuwaona wale ndege, ndipo sasa kikatokea kishindo
kingine cha lile lori la ng’ombe, nakumbuka nilikimbia kurudi
nilikotoka, nikarudi baadaye nikiwa natetemeka sana,” alisema Zuwena.
Orodha ya majina ya majeruhi na waliofariki kutokana na ajali hiyo
Ajali hiyo ilitokea alfajiri ya Jumatano
iliyopita ambapo watu wanne walifariki, watatu eneo la tukio na mmoja
alipoteza maisha baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Amana, Ilala
jijini Dar es Salaam.

Note: Only a member of this blog may post a comment.