Imelda Mtema
Mtangazaji wa Kipindi cha
‘Wanawake Live’ kinachorushwa kupitia Televisheni ya East Africa, Joyce
Kiria amefunguka kuwa hata kama mumewe wa ndoa hatakuwa mchapakazi
atampiga chini na kuendelea na maisha mengine.
“Kwangu, hata kama mume naye atakuwa
mzembe wa kupiga kazi nampiga chini kabisa maana sasa hivi tunakimbizana
na kazi ya kupiga kazi kwa nguvu ili tuwezeshe kusonga mbele zaidi,”
alisema Joyce.
Pia mtangazaji huyo aliongeza kuwa
anawaomba wanawake wengi wajitokeze kwani hakutakuwa na kiingilio
chochote, lengo ni kuja kujifunza mbinu za kujikomboa kama wanawake na
kujiamini katika kufanya kazi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.