Brazil ni nchi pekee ambayo imebarikiwa kuwa na vipaji vingi vya
mpira, lakini hata Afrika pia imebarikiwa kuwa na wachezaji wenye vipaji
vya mpira ambao wanatikisa ulimwengu.
Mchezo wa mpira ni miongoni mwa michezo inayolipa vizuri wachezaji
wake, wanapata mpaka jeuri ya kuendesha magari ya kifahari na kuishi
maisha ya juu kama wafalme.
Afrika imebarikiwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vikubwa lakini pia
wamejipatia fedha nyingi kupitia mchezo huo. Wachezaji wengine kutoka
Afrika wanalipwa fedha nyingi kuliko hata wachezaji kutoka mabara ya
Ulaya na Amerika.
Hawa ni miongoni mwa wachezaji wa Afrika ambao wamefanikiwa kuwa na utajiri mkubwa zaidi.
Samweli Eto’o
Eto’o raia wa Cameroon, ni miongoni mwa wachezaji wachache duniani
waliopata bahati ya kucheza kwenye timu nyingi kubwa duniani. Aliwahi
kucheza kwenye timu kadhaa kubwa zikiwemo Real Madrid, Barcelona, Inter
Milan, Chelsea, n.k.
Eto’o anaongoza kwenye list ya wachezaji matajiri kutoka Afrika akiwa
na utajiri wa $202 milioni. Utajiri wa Eto’o uliongezeka pale alipotua
kwenye timu ya Anzhi Makhachkala, ya nchini Urusi ambapo alikuwa
analipwa dola milioni 25 kwa mwaka.
Pia ana biashara kibao ambazo zinamuingizia fedha nyingi. Ana miliki
mtandap wa simu nchini Cameroon pamoja na academy za mpira wa miguu,
licha ya kuwa na utajiri wote amefungua kituo cha Samweli Eto’o
Foundation nchini Cameroon kwa kuisaida jamii.
Eto’o kwa sasa ni mchezaji wa Antalyaspor inayoshiriki ligi kuu ya
nchini Uturuki, ameshacheza mechi 24 kwenye timu hiyo na kufanikiwa
kufunga magoli 16.
Yaya Toure
Yaya Toure amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa miaka mitatu
mfululizo kuanzia mwaka 2011-2014. Ni mmoja kati ya kizazi bora kuwahi
tokea kwenye historia ya soka ya nchini Ivory Coast.
Toure amefanikiwa kuwa na utajiri wa $170 milioni, huku akiwa
anaendelea kulipwa dola milioni 15 kila mwaka na timu yake ya Manchester
City akiwa ndiyo mchezaji anayelipwa hela nyingi kwenye timu hiyo.
Kwa sasa Toure ni mmoja kati ya viungo bora duniani ambao wanafanya
vizuri, ameshacheza mechi 188 akiwa na Manchester City na kufunga magoli
54.
Didier Drogba
Mafanikio ya Drogba yalianza kuonekana kuanzia mwaka 2004 alipojiunga na timu ya Chelsea akiwa na umri wa miaka 26.
Drogba ni mmoja kati ya wachezaji matajiri Afrika akiwa na utajiri wa
wa $155, utajiri wake ulianza kukua alipojiunga na Chelsea alikuwa
analipwa mshahara wa dola 170,000 kwa wiki.
Timu ya Shanghai Shenhua ndiyo ilitanua zaidi akaunti ya Drogba pale
walipo msajili mwaka 2012 na kumlipa mshahara wa dola 320,000 kwa wiki,
na baadaye timu ya Galatasaray ilimchukua na kumlipa mshahara wa $5.2
milioni kwa mwaka. Pia drogba anamiliki miradi kibao ambayo bado
inaendelea kumuingizia fedha nyingi ambazo zitaendelea kuingia hata
akiamua astaafu kucheza mpira.
Drogba kwa sasa anacheza ligi ya Marekani maarufu kama Major League
Soccer (MLS), kwenye timu ya Montreal Impact akiwa mpaka sasa kacheza
mechi 11 na kufunga magoli 11.
Wachezaji wengine matajiri Afrika ni; Jay-Jay Okocha : $150m, Nwankwo Kanu : $100m, Michaël Essien/Panathinaïkos : $70m, Emmanuel Adebayor/Libre : $57m, Obi Mikel/Chelsea : $50m, Kolo Touré/Liverpool : $43m, Sulley Muntari/Al-Ittihad : $40m.
Note: Only a member of this blog may post a comment.