Mtoto Latifah Nasbu ‘Tiffah
Musa Mateja, AMANI
DAR ES SALAAM! Hii ni EXCLUSIVE stori!
Kufuatia kelele kibao kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba mtoto wa staa
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, yaani Latifah ‘Tiffah’ aliyemzaa
na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ si wa nyota huyo, hatimaye, jamaa
ameamua kupima vinasaba ‘DNA’ (DeoxyriboNucleic Acid).
ISHU ILIKUWA AFRIKA KUSINI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Diamond aliamua kutekeleza mpango huo nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambako aliamini hakuna ‘macho mengi’ ya watu, hususan mapaparazi.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
SIKIA HII
“Jamani mimi nataka niwape stori ambayo ni ya uhakika. Hivi mnajua kwamba Diamond aliamua kwenda Sauzi kupima DNA yake na mtoto wake Tiffah?
“Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisufigisu, akamwambia Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye. Ni kabla hajaenda Marekani.”
MAJIBU HAYA HAPA
Chanzo hicho kikasema: “Majibu ya DNA yamesema, Nasibu Abdul ni biological father (baba wa damu) wa mtoto Tiffah. Ilibidi jamaa amwage chozi maana alifikiria mengi, watu wamesema sana kuhusu yeye na Tiffah, kwamba si mwanaye, mara ni mtoto wa Ivan (Ssemwanga, mtalaka wa Zari), mara ni mtoto wa pedeshee mmoja wa Bongo. Yaani mengimengi yalisemwa.”
MAMA DIAMOND ASHANGAZWA
Chanzo hicho kikazidi kuweka wazi kwamba majibu hayo ya DNA yalimshangaza mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ hasa kutokana na maneno yaliyosambaa katika jamii, kwamba kijana wake huyo alibambikwa mtoto.

Mtambo wa DNA
DIAMOND NA AMANI
Baada ya madai hayo, gazeti hili lilijihangaisha kwa kuzingatia weledi ili kumpata Diamond mwenyewe kwa lengo la kumpa nafasi ya kujieleza kama taaluma inavyotaka kwamba anasemaje kuhusu kuwepo kwa habari hii mpya kabisa ya kupima DNA.

KUMSIKIA DIAMOND, BONYEZA HAPA
“Yeah! Unajua watu wamesema sana. Wametunga sana, mimi sikuwa na
wasiwasi, niliamini mtoto ni wangu, ila ili kujiridhisha zaidi nikasema
niende nikapime DNA yangu na ya mtoto.
“Tiffah ni mtoto wangu kabisa, nimefurahi kwa majibu. Ndiyo maana sasa nimejiachia, ukifika ofisini kwangu nimeweka picha zake kwenye fremu. Sina wasiwasi kabisa mimi si mtu wa mikono kichwani tena.”

MAHOJIANO
Amani: “Ni kweli ulitoa machozi?”
Diamond: “Siyo ishu, kama unaishi katika nchi yenye baadhi ya watu wanaozusha maneno kama yale halafu unagundua ni uzushi wao tu, kulia ni nini?”
Amani: “Unasema tangu awali ulijua Tiffah ni mtoto wako, kwa nini uliamua kwenda kupima DNA?”
Diamond: “Utamaduni wa kutopima ni sisi Wabongo tu, wenzetu mbele siyo ishu. Ni kujiridhisha kwa asilimia mia moja tu. Bongo ukimwambia mwenzio mkapime DNA ya mtoto, anaweza kukujia juu kwamba humwamini.”
KUHUSU PEDESHEE KUDAIWA NDIYE BABA WA MTOTO
Diamond: “Nimesikia wakisema hivyo, lakini mimi nataka kuwaambia kwamba, huyo pedeshee (jina lipo) hajawahi kuwa mtu wa Zari. Mimi ndiye ninayejua nini kilitokea! Hao wanaosema waache waseme tu.”
Amani: “Nini kilitokea? Gusia kidogo tafadhali.”
Diamond: (kwa tabu sana), “kifupi nilimzidi jamaa mahesabu, mimi nikaondoka na Zari. Ndiyo maana leo hii nampa heshima kwa sababu hakuwahi kufanya lolote hapa Bongo.”
KUHUSU IVAN
Amani: “Wanaposema Tiffah ni mtoto wa Ivan, wewe unachukuliaje?”
Diamond: “Ingewezekana vipi! Watu watofautiane, miaka ipite halafu waseme mtoto ni wake! Mimba inakaa tumboni kwa miaka mingapi?”
MAMA DIAMOND AMEANZA MAMBO YAKE
Juzi, Amani lilimpigia simu mama Diamond kwa lengo la kumuuliza kuhusu alivyojisikia baada ya majibu ya DNA kuonesha kuwa, Tiffah ni mjukwuu wake kabisa lakini simu yake iliita bila kupokelewa, licha ya kupigwa mara kadhaa. Tabia ya kutopokea simu alikuwa nayo zamani, hapo katikati akaiacha. Inaonekana ameirudia tena!

Note: Only a member of this blog may post a comment.