Barakah Da Prince
Nyemo Chilongani
Mwanamuziki anayekuja kwa kasi kwenye
Muziki wa Bongo Fleva, Barakah Da Prince ameamua kumpoza mwanamuziki
mwenzake, Sunday Mjeda ‘Linex’ baada ya stori kuenea mitandaoni kwamba
alivunja amri ya sita na mchumba wa Linex mara baada ya picha
iliyomuonesha msichana huyo akiwa na mwanaume aliyefanana na Barakah.
Sunday Mjeda ‘Linex’
Akichonga na gazeti hili kwa njia ya simu Barakah alisema kwamba mara
ya kwanza alipozisikia stori hizo, alishtushwa nazo kwani anamheshimu
sana Linex na hawezi kufanya hivyo kutokana kuwa na ukaribu naye na hata
huyo mwanaume, amefanana naye tu na si yeye.
“Nilishtushwa nilipozipata stori hizo.
Siwezi kufanya upuuzi huo, namheshimu Linex, mwanaume yule si mimi,
labda tumefanana tu. Najiheshimu na hata huyo msichana simfahamu
kabisa,” alisema Barakah.

Note: Only a member of this blog may post a comment.