Katika ukurasa wake wa Instagram Faiza ameandika huku akiwapondea wale wanaomsikitikia, na kusema kuwa Chid amejichagulia mwenyewe kuwa hivyo kwani kabla hajaanza kutumia alikuwa anafahamu madhara yake.
“Kila mtu anamsikitikia Chidi kwa nini? Chidi sio mtoto ni maisha aliyo chagua, pengine unaweza kumsikitia mtoto aliye jifunza akiwa chini ya miaka 18 lakini sio mtu mzima! Kila siku mifano tunaiona jinsi gani madawa yana haribu watu inaama hawaoni ? Hawasikii ?"Faiza ameendelea kuandika
"Hapana kwa kweli mimi naona unavuna unachokipanda. Unapo sema ugumu wa maisha ndiyo umekupeleka kuvuta madawa au kuuza - hivi mnazani wote tunao cheka maisha yetu mepesi? Kwa kweli ni uzembe......! acheni kabisa kuwahurumia watu kijinga, lazima wajue wamekosea sio kuwa peti peti”.
Pamoja na hayo Faiza ameonekana kuchukizwa na kitendo cha biashara ya madawa ya kulevya inayoendelea nchini, na kutaka watumiaji na wauzaji pia wafungwe iwapo watathibitika, ili kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya.
“Hivi kwa nini wanao nunua madawa pia wasifungwe ??? Kwa sababu mtazamo wangu unaona mnunuzi na muuzaji wote ni wahalifu!
Kati ya hawa watu wawili wote wanafanya biashara maana kama hamna mnunuzi hakuna muuzaji, kama hakuna muuzaji hamna mnunuzi”, aliandika Faiza.
Pamoja na hayo Faiza amemtakia heri Chidi Benzi katika mapambano yake na kuachana na madawa ya kulevya, ili aweze kurudi kama zamani.
Note: Only a member of this blog may post a comment.